Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi EACC imezindua warsha ya siku tano ya kukabiliana na ufisadi ambao umekithiri kwenye utoaji zabuni.

Warsha hiyo yenye mada “Kuimarisha Maadili katika Ununuzi wa Umma,” imeandaliwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Kenya ya Usimamizi wa Ugavi KISM katika kaunti ya Mombasa.

Uzinduzi huo umejiri huku kukiwa na kashfa nyingi za ufisadi nchini, ambapo fedha za umma zimeporwa kupitia taratibu mbovu za utoaji zabuni.

Kulingana na takwimu kutoka kwa EACC, udanganyifu wa ununuzi unachangia hadi 80% ya kesi zote za ufisadi zinazochunguzwa na tume hiyo.

June 12, 2023