Eneo la magharibi mwa kenya linaongoza katika visa vya unywaji wa pombe haramu nchini ikifuatwa na maeneo ya pwani na kati.

Haya ni kwa mujibu wa ripoti iliyozinduliwa leo na mamlaka ya kitaifa ya kampeni dhidi ya unywaji wa pombe haramu na dawa za kulevya NACADA.

Kulingana na afisa mkuu wa NACADA Victor Okioma,ongezeko la uraibu wa pombe limechangiwa pakubwa na kuhalalishwa kwa matumizi ya baadhi ya pombe za kitamaduni.

Ripoti hiyo pia imebaini kuwa vijana wengi wanaanza kunywa pombe wakiwa na umri mdogo.

Kwa upande wake katibu katika wizara ya usalama Raymond Omollo amesema kuwa serikali haitolegeza kamba katika kupambana na kero hii.

May 12, 2023