BY ISAYA BURUGU,15TH JULY,2023-Mamlaka ya kudhibiti bei za kawi nchini EPRA imetangaza bei mpya za bidhaa za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta taa wiki mbili baada ya bei za awali.Katika tangazo ambalo limetolewa jana jioni, bei ya petroli imepungua kwa shilingi 0.85 huku bei ya dizeli ikisalia jinsi ilivyo na ile ya mafuta taa ikipungua kwa shilingi 3.96.

IFAHAMIKE KUWA  Julai mosi, EPRA waliwashangaza  Wakenya kwa kutangaza ongezeko la bei ya bidhaa hizo muhimu kwa bei ya juu Zaidi kuwahi kushuhidwa nchini.Bei ya petroli iliongezeka kwa shilingi 13.49 huku ile ya dizeli ikiongezeka kwa shilingi 12.39 na mafuta taa ikaongezeka kwa shilingi 11.96.

Hii iliweka maisha ya wengi kuwa magumu kwani jijini Nairobi, Petroli ilianza kuuzwa kwa shilingi 195.53 kwa lita, dizeli ikiuzwa kwa shilingi 179.67 kwa lita na mafuta taa ikiuzwa kwa shilingi 173.44 kwa lita.

Hata hivyo, bei hizi mpya zilipata pingamizi kali kutoka kwa Wakenya wengi ambao walihisi ni mzigo mkubwa ambao umetwikwa mabegani mwao kutokana na kupitishwa kwa mswada wa fedha 2023.

 

 

 

July 15, 2023