Katibu katika Idara ya urekebishaji wa tabia nchini Esther Ngero amejiuzulu, siku saba baada ya uhamisho wake kutoka kwa ofisi ya mkuu wa baraza la Mawaziri Musalia Mudavadi.
Ngero amekua afisa wa kwanza wa serikali kujiuzulu kwa kile alichokitaja kama sababu za kibinafsi. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kutoka kwa ofisi ya rais na mkuu wa utumishi wa Umma Felix Koskei, Bi. Ngero aliwasilisha ombi la kujiuzulu lililopokelewa na kuidhinishwa na rais.