Familia ya marehemu Edward Morema na mkewe Grace Mong’ina Morema waliouawa na watu wasiojulikana nyumbani kwao Nyamakoroto inataka uchunguzi uharakishwe ili wahalifu hao waweze kutiwa mbaroni.

Kulingana na ripoti ya uchunguzi wa maiti hizo mbili uliofanyika katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Kisii Bw. Morema alipigwa na kifaa butu mara mbili kichwani na kupata majeraha matatu ya kisu kwenye mbavu zake huku mkewe akifariki dunia kwa kunyongwa.

Wahalifu hao waliharibu camera za CCTV zilizokuwa katika nyumba hiyo.

Kamanda wa polisi wa Kaunti ndogo ya Masaba Kaskazini Robert Ndambiri alisema maafisa bado wanawazuilia wafanyakazi wawili katika boma hilo, ambao wanasaidia katika uchunguzi.

April 1, 2023