Lusaka

Gavana wa Kaunti ya Bungoma Kenneth Lusaka amechaguliwa na baraza la magavana kuongoza kamati ya magavana kumi watakaosaida kufanikisha mazungumzo kati ya upande wa serikali na viongozi wa upinzani ili kutuliza joto la kisiasa linaloendelea nchini. Viongozi waliopendekezwa na magavana nchini wanajumuisha:

Anne Waiguru,

Ahmed Abdullahi

Stephen Sang,

Kenneth Lusaka,

Fatuma Achani;

Mutahi Kahiga,

Simba Arati,

Joseph Ole Lenku,

Wavinya Ndeti na

Gavana Ochillo Ayacko.

Katika taarifa yake jioni ya leo, baraza la magavana limeeleza wasiwasi wao kuhusu kuendelea kwa mgongano wa kisiasa unaoshuhudiwa kwa sasa nchini, kabla ya kuamua kuunda kamati hiyo kusaidia katika katika mashauriano na viongozi kutoka pande zote mbili.

https://twitter.com/KenyaGovernors/status/1653407070123696130?s=20

May 2, 2023