BY ISAYA BURUGU 27TH DEC 2022-Gavana wa kaunti ya Meru Kawira Mwangaza amekanusha madai ya ukiukaji sheria dhidi yake yaliyotolewa na wawakilishi wadi wa kaunti hiyo na kutumiwa kama msingi wa kumangatua mamlakani.Kawira amefika mbele ya kikao maalum cha bunge la seneti kilichobuniwa kuchunguza swala hilo. Gavana huyo amesomewa mashataka yote yakiwemo ukiukaji katiba kupitia kumteua mumewe kama msimamizi wa maswala ya vijana na kutofuata sheria katika utekelezaji wa majukuu yake.
Mwenyekiti wa jopo hilo Seneta kakamega Bonny Khalwale ameridhia ombi la gavana Mwangaza kuwasilisha Ushahidi Zaidi anaodai ndio utakaofichua dhana potovu ya MCA wa Meru dhidi yake.Vilevile bunge la kaunti ya Meru limepewa fursa kuwasilisha tetesi na majibu yake kufikia mwisho wa hivi leo.Wakili wa MCA wa Meru Muthomi Thiankolu akipinga hatua ya gavana Mwangaza kuruhusiwa kuwasilisha Ushahidi akidai huenda wateja wake hawatapata muda kudadisi ushidi huo na kujibu kam ainavyostahili.
Wakili Elias Mutuma anamwakilisha gavana Mwangaza .Vikao hivyo vinaendelea huku gavana Mwangaza akitarajiwa kujitetea kesho. Kamati hiyo inatarajiwa kuchukua mapumziko Alahamisi juma hili ili kutayarisha ripoti yake ya mwisho kabla ya kuiwasilisha kawa Seneti Ijumaa wiki hii.
Wakati huo huo viongozi wa dini ya kiislamu eneo la kasakzini mwa boinde la ufa wanawataka wawakilishi wadi wa Meru kumpa wakati gavana Mwangaza kutekeleza jukumu lake.Wakiongozwa na mwenyekiti wao Shelkh Abubakari Bini,viongozi hao wanasema itakuwa ni bora kwa MCA hao kusikiliza sauti ya wananchi na kumruhusu gavana Kawira kuwatekelezea wananchi kazi.