Majibizano yamezuka kati ya gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja na mwenzake wa Kisumu Prof. Anyang’ Nyong’o kuhusu kuandaliwa kwa maandamano katika kaunti hizo mbili.

Katika taarifa yake mapema leo, Gavana Nyong’o alitangaza kuwa kaunti hiyo haitaandaa maandamano mengine ya kupinga uongozi wa serikali, na badala yake kusema kuwa wataungana na wenzao katika jiji la Nairobi ili kuendeleza maandamano hayo.

Hatua hii hata hiyo haikupokelewa vizuri na gavana Johnson Sakaja, ambaye alijibu kwa waraka sawia, huku akisema kwamba maandamano haya yamesababisha hasara kubwa katika jiji la Nairobi na kwamba hayatakubalika tena katika jiji hilo.

Sakaja aidha alimwomba gavana Nyongo kutoleta maandamano katika jiji la Nairobi ambalo lina hudumia mamilioni ya wakenya kutoka pembe zote za taifa.

Gavana Nyong’o hata hivyo amerejelea uamuzi huo na kutangaza kwamba maandamano hayo yataendelea kama yalivyoratibiwa Alhamisi hii ya tarehe 30.03.2023. Chapisho la gavana Nyong’o kubadili msimamo wake liliambatanana kauli Vox Populi, Vox Dei !” inayomaanisha kwamba Sauti ya watu, sauti ya Mungu!.

March 29, 2023