Gavana wa Narok Patrick Ntutu amezindua shehena ya pili ya dawa ambayo itasambazwa kwa hospitali na zahanati mbalimbali katika kaunti ya Narok. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo katika hospitali ya rufaa ya Narok Ntutu amedokeza kuwa serikali yake inapania kuimarisha huduma za matibabu kwa kuanzisha mpango wa kutoa dawa za bure kwa wakaazi wa Narok.
I later proceeded to Narok Referral Hospital to flag off the second batch of medicine. My government will strive to ensure adequate free medicine in all Hospitals and Medical Centres for the people of Narok. pic.twitter.com/uEoVbLdz6C
— Governor Patrick Ole Ntutu (@OleNtutuK) October 26, 2022
Aidha gavana huyo amewaonya wafanyakazi wa hospitali wanaochukua dawa bila idhini hali inayochangia uhaba wa dawa katika hospitali hiyo ya rufaa na hospitali zinginezo kaunti ya Narok. Kufikia sasa serikali ya Narok imetoa jumla ya dawa milioni 92.
I have reiterated that we will take serious measures against anyone who fraudulently tries to acquire these drug because they are meant for the people of Narok. pic.twitter.com/NlCjvCKVGi
— Governor Patrick Ole Ntutu (@OleNtutuK) October 26, 2022