Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja amesema kuwa jiji kuu litashuhudia hasara kubwa ya mapata iwapo maandamano yaliyoandaliwa na muungano wa upinzani yataendelea.
Sakaja aliyekuwa akizungumza mapema leo Jumanne, Machi 21 wakati wa uzinduzi wa wimbi la pili la Mpango wa Rapid Results Initiative, alisema Kaunti ya Nairobi ilikusanya mapato ya Shilingi milioni 30.3, ambayo ni nusu kiwango cha mapato yanayokusanywa kila siku.
Gavana huyo ametoa wito wa mashauriano kati ya serikali na Upinzani, akisema kuwa hali ikiendelea hivi itasitisha shughuli za maendeleo kwa kiwango kikubwa katika siku za usoni, kutokana na kupungua kwa mapato.
Launched our second wave of Rapid Results for sectors this morning at City Hall. The delivery areas range from lighting, roads, health, housing, education, water among others with specific outcomes for the next 100 days. Lazima iWork. pic.twitter.com/RGCknGTA2m
— Sakaja Arthur Johnson (@SakajaJohnson) March 21, 2023