Vikao vya kusikiliza hoja ya kumbandua gavana wa Kaunti ya Meru Kawira Mwangaza, vimeng’oa nanga asubuhi ya leo katika bunge la seneti. Maseneta wamepata fursa ya kusikiliza na kuangazia ushahidi utakaowasilishwa na wawakilishi wadi wa meru dhidi ya Gavana Mwangaza, huku naye Gavana mwangaza ambaye alikuwa katika hali sawia mwishoni mwa mwaka jana, akitarajiwa kupata fursa ya kujitetea dhidi ya shutma za wawakilishiwadi hao.
Maseneta baadaye watafanya maamuzi ya kumtimua au kumrejesha ofisini gavana huyo, ambaye aliponea shoka sawia mwezi disemba mwaka jana.
Aidha Gavana huyo amekanusha mashtaka yanayomkabili katika kikao kinachoendelea katika bunge la seneti cha kumuondoa madarakani.
Kawira alisomewa mashtaka saba anayokabiliwa nayo ambayo aliyakana kabisa, na hivyo kumfungulia njia wakili wake Elisha Ongoya kumtetea.Mashataka yanayomkabili ni pamoja na Ufujaji wa rasilimali za kaunti kwa kutumia jamaa zake,upendeleo, kuwatukana na kuwadhalilisha viongozi wengine miongoni mwa mashataka mengine.
Hata hivyo wakili huyo wa Mwangaza alitupilia mbali mashtaka hayo akiteta kuwa mteja wake hana hatia na walalamishi hawana kesi thabiti dhidi ya gavana huyo.