Kawira Mwangaza - seneti

Gavana wa Kaunti ya Meru, Kawira Mwangaza, atapata fursa ya kujitetea mbele ya Bunge la Seneti wiki ijayo, baada ya bunge hilo,kutenga muda wa kusikiliza hoja ya Kumbandua.

Bunge la Seneti limetenga siku za tarehe saba na nane mwezi Novemba kwa ajili ya kusikiliza mswada wa kumbandua gavana Mwangaza kutoka kwa wadhifa wake katika uongozi wa Kaunti ya Meru.

Maseneta katika kikao cha Alhamisi, waliidhinisha pendekezo la kumruhusu gavana Mwangaza kujitetea mwenyewe mbele ya bunge, baada ya pendekezo la seneta wa Narok, Ledama Ole Kina, la kuundwa kwa kamati iliyopendekezwa hapo awali kukataliwa na maseneta.

SOMA PIA: Mahakama ya Nyeri Yakataa kusimamisha mjadala wa Kumbandua Gavana wa Meru.

Gavana huyo alibanduliwa kutoka kwa wadhifa wake na bunge la Kaunti ya Meru mwishoni mwa mwezi uliopita. Hata hivyo, hatua hii inaweza kubadilishwa ikiwa gavana na mawakili wake wataweza kutoa ushahidi mwafaka utakaowashawishi maseneta.

 

November 2, 2023