Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ntutu asubuhi ya leo alipokea ripoti ya ukaguzi wa ofisi ya HR na Mishahara kutoka taasisi AGMOND International iliyofanya ukaguzi huo.

Akizungumza katika ofisi za kaunti, Ntutu alisema kuwa zoezi hili la ukaguzi wa wafanyikazi lilianza mwezi Mei mwaka jana kwa lengo la kufahamu rekodi za wafanyikazi, kuoanisha kazi na rasilimali, na kuboresha ufanisi wa udhibiti wa ndani na mifumo ya Serikali ya Kaunti.

January 17, 2024