BY ISAYA BURUGU,21ST JAN 2023-Gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ameshinda raundi ya kwanza ya kesi ya kupinga uteuzi maafisa wakuu kumi wa serikali ya kaunti waliozinduliwa wiki jana.Hii ni baada ya mahakama ya leba kule Mombasa kudinda kutoa agizo kuzuia mchakato wa kuwaidhinisha maafisa hao wakuu kuanza kutekeleza jukumu lao.
Gavana Abdulswamad Nassir alikuwa amewateua mawaziri kumi katibu wa kaunti ,mkurugenzi mkuu wa bodi ya huduma kwa umma ya Mombasa na washauri kadhaa kumsaidia kuongoza.
Hata hivyo wakaazi wanne wa Mombasa Abdullmajid Ali Busayyid, Mesh Mwaniki, Maria Magdalene Fernandes, na Mohammed Mohsin Abdulkarim,walikwenda mahakamani chini ya ombi la dharura wakitaka kuzuia mchakato wa kuwaajiri maafisa hao.
Wanne hao kupitia wakili wao David Maseke wa Shabaan Associates LLP, walisema gavana huyo alikiuka sheria katika uteuzi huo.