BY ISAYA BURUGU,28TH SEPT,2023-Aliyekuwa mkuu wa sheria profesa Githu Muigai amesema kuwa watalamu mbali mbali kutoka kwenye Nyanja tofuati  wanapaswa kushirikishwa katika kubuni tume ya uchaguzi nchini.

Muigai akizungumza katika kikao cha  kamati ya uiano inayongozwa na wawakilisha wa marengo ya Azimio la Umoja One Kenya na Kenya Kwanza katika ukumbi wa Bomas,jijini Nairobi,amesema kuwa tofauti na hali ilivyokuwa kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2007/8 uliokumbwa na utata ambapo tume ya uchaguzi iliteuliwa kutumia mfumo wa kutaja makamishna,kuelekea mbele ni sharti watalamu kuhusishwa.

.Muigai pia amezamia swala la hitaji la kutaka uchaguzi wa mwaka jana kufanyiwa ukaguzi, ambapo amesema haitakuwa bora kufanya ukaguzi kw alengo la kubadili matokeo lakini kuboreshwa kwa mfumo wa uchaguzi kwa minajili ya siku zijazo.

. Vikao hivyo vinaendelea chii ya uongozi wa vionara  wa Kimani Ichungwa na Kalonzo Musyoka.

 

 

 

September 28, 2023