BY ISAYA BURUGU 5TH OCT 2023-Viogozi mbali mbali akiwemo aliyekuwa diwani wa eneo la Ololulunga Jackson Kamoye wameunga mkono serikali kwa juhudi zake za kuwafirusha watu kutoka msitu wa mau.
Kamoye ambaye ni mwenyekiti wa shirika la Friends of Mau amesema msitu wa mau ni chemi chemi ya maji na ni lazima ilindwe kikamilifu.
Usemi wa viongozi hao unajiri huku rais Wiliam Ruto na Waziri wa mazingira Suipan Tuya wakiapa kuendeleza harakati za kulinda misitu nchini kama sehemu ya juhudi za kuafikia asilimia hitajika ya msitu.Serikali inalenga kupanda miti bilioni 15 kufikia mwaka 2030.Mwanahabari wetu Antony Mintila ana mengi Zaidi.