BY ISAYA BURUGU,10TH FEB,2023-Hazina ya kitaifa ya malipo ya uzeeni NSSF sasa inawataka waajiri kuheshimu mara moja agizo la mahakama linalowataka kuongeza kiwango cha fedha wanazowatoza wafanyikazi wao kuelekea kwenye hazina hiyo kila mwezi.
Kupitia taarifa iliyotolewa leo mwenyekiti wa hazina hiyo Antony Munyiri waajiri wamekuwa wakitimiza sheria nambari 45 ya mwaka 2013 na wanapasw akuendelea kufanya hivyo huku akiwataka wasiofanya hivyo kuanza kufanya hivyo mara moja
.Ada hizo mpya zitapelekea mwajiri na mfanyikazi wake wakichangia shilingi 2160 kutoka kiwango cha sasa cha shilingi mia mbili.Kwa mjibu wa NSSF kila mwajiri atahitajika kulipa ada hizo mpya kufikia tarehe tisa kila mwezi.
Haya yanajiri baada ya majaji watatu wa mahakama ya rufaa, Hannah Okwengu, Mohamed Warsame naJohn Mativo kubatiliza agizo lililotolewa na mahakama kuu mnamo septemba mwaka jana lililokuwa limetangaza sheria ya NSSF yam waka 2013 kuwa kinyume cha katiba,kwani wananchi hawakuhusishwa .