Kiongozi wa taifa Rais William Ruto amewatoa wito kwa idara za magereza nchini kushirikiana na serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa taifa.

Rais aliyezungumza katika halfa ya 26 ya kufuzu kwa maafisa wa magarereza katika Chuo cha Mafunzo cha maafisa wa Magereza eneo la Ruiru kaunti ya Kiambu, alisifia ongezeko la idadi ya wanawake waliofuzu mwaka huu, akisema kwamba idadi hii inafaa kuimarika hata Zaidi katika siku za usoni. Mahafali 222 katika kiwango cha Cadet wamefuzu katika hafla ya leo.

Kuhusiana na maswala ya kuimarisha uchumi wa taifa, Rais ameahidi kuiboresha sekta ya magereza kwa kuipa tinga 67 ili kuiwezesha kujihuisha ifaavyo katika uzalishaji wa chakula nchini, Pamoja na kuwekez akatika kushirikisha idara hii katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

April 24, 2023