Kama njia mojwapo ya kupunguza idadi ya wafungwa katika magereza ya humu nchini, jaji mkuu Martha Koome amesema kuwa idara ya mahakama imejitolea kupitia upya hukumu za wafungwa ili kuwaachilia wafungwa wa makossa mdogo kufanya huduma za jamii badala ya kutumikia kifungo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua zoezi la kupunguza idadi ya wafungwa magerezani, Koome amedokeza kuwa katika mwaka wa fedha uliopita, 2023/2024, mahakama zilipitia hukumu 6,555 na Kati ya hizi, watu 2,918 waliachiliwa chini ya maagizo ya kuitumikia jamii.

 

Aliongeza kuwa Pia idara hiyo ya mahakama inatekeleza hatua za muda mrefu ili kuzuia kuzuiliwa kwa lazima kwa watu wasio na hatia huku akishikilia kuwa Sera ya Dhamana itaendelea kutekelezwa kote nchini ili kupunguza idadi ya watu wanaoshikiliwa kwenye seli na rumande.

August 12, 2024