BY ISAYA BURUGU 9TH FEB,2023-Inspekta Jenerali wa polisi Japhet Koome siku Alhamisi alikanusha madai kwamba maafisa wake walienda kwenye nyumba ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiangí huko Karen.Alisema aliangalia na kugundua kwamba hakuna operesheni kama hiyo iliyoidhinishwa na idara yake.Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi Twalib Mbarak pia alikanusha kuwa maafisa wake walihusika katika jaribio hilo la usiku wa Jumatano.

Hii ilitokana na ripoti kwamba kundi la maafisa wa polisi lilijaribu kufikia nyumba ya waziri wa zamani mtaani Karen Jumatano usiku.Maafisa hao waliofika kwa magari mawili ambayo hayakuwa na namabari za usajili walidai kutoka EACC na Halmashauri ya Urejeshaji Mali ya Umma (ARA).

Maafisa wa ARA pia walikanusha kuwa walitume mtu yeyote kwa boma la Matyang’i.Kukanusha kwa vyombo vya dola kwa jaribio hilo la uvamizi kuliwaacha wengi wakijiuliza ni akina nani waliokuwa nyuma ya tukio hilo.

Walioshuhudia walisema maafisa hao walifika hapo mwendo wa saa nne usiku. Wakati huo kulikuwa na wanasheria na marafiki katika nyumba ya Matiang’i.

 

 

February 9, 2023