Mamlaka Huru ya kutathmini utendakazi wa Polisi IPOA inachunguza visa viwili vya madai ya ukatili wa polisi vilivyotokea Kisumu na Nairobi wakati wa maandamano ya kuipinga serikali.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa Mamlaka hiyo, Anne Makori, maafisa wa IPOA waliotumwa kote nchini kufuatilia mienendo ya maafisa wa polisi walibaini kisa cha Kisumu ambapo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha maseno aliuawa kwa kupigwa risasi.
Kulingana na IPOA, kwingineko jijini Nairobi, raia mmoja alidaiwa kujeruhiwa vibaya na polisi katika Soko la Toi.
Aidha IPOA pia ilibaini kuwa maafisa wengine walijeruhiwa wakati wa maandamano ya siku nzima ambayo pia yalisababisha uharibifu wa mali.
IPOA statement on monitoring of police conduct during the Azimio demonstrations. ^DD pic.twitter.com/ZK4T9NZSvP
— IPOA (@IPOA_KE) March 21, 2023