Jeremiah Kioni bado anaaminika kuwa Katibu Mkuu halali wa chama cha Jubilee kulingana na utafiti uliofanya na TIFA.
Katika utafiti huo uliotolewa leo Alhamisi, asilimia 32% ya waliohojiwa wanamtambua Kioni kama katibu mkuu wa Jubilee huku 21% wakimchukulia Kega kama katibu mkuu wa chama hicho.
Kati ya wanaoamini uongozi wa Kioni, 28% wanaunga mkono serikali, 47% wanaunga mkono upinzani na 17% wanaunga mkono upande wowote. Kwa upande mwingine, 31% wanaoamini katika uongozi wa Kega wanaunga mkono serikali, 15% wanaunga mkono serikali na 13% hawana upande wowote.
TIFA ilisema zaidi kwamba asilimia 37 ya waliohojiwa wanataka wale ambao walichaguliwa kwa tikiti ya Jubilee lakini wakahamia Muungano kenya kwanza wanapaswa kujiuzulu na kuomba kuchaguliwa tena kwa Tikiti ya chama cha UDA.
Aidha asilimia 39 wanaamini kuwa wabunge hao wanapaswa kusalia tu katika chama cha Jubilee huku 18% wakihifadhi maoni yao. Utafiti huo wa kitaifa ulifanyika kuanzia tarehe 24 hadi 30 Juni, 2023 ambao ulijumuisha wahojiwa 1,530.
State of Kenyan politics, bipartisan talks, and political alignment.Perceived legal secretary general of Jubilee party. #TifaPolls pic.twitter.com/zQcl8X1QnL
— TifaResearch (@TifaResearch) September 21, 2023