Mwanahabari Jackie Maribe amepata afueni baada ya mahakama kumondolea mashtaka ya mauaji yaliyokuwa yakimkabili huku mshtakiwa mwenzake Joseph Irungu maarufu Jowie akipatikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani mnamo mwaka wa 2018.

Jaji Grace Nzioka akisoma hukumu hiyo mapema leo, alieleza hakuna ushahidi ulioonyesha kuwa Maribe alikuwa na nia ya kumuua marehemu kimani huku Jowie akipatikana na makosa ya mauaji kufuatia ushahidi wa kutosha uliotolewa.

Jowie kwa sasa anazuiliwa kwenye rumande hadi tarehe 8 mwezi ujao baada ya jaji Nzioka kufutilia mbali bondi aliyokuwa amepewa.

Akizungumza muda mfupi baada ya hukumu kutolewa, Maribe alitumia maneno ya bibilia kutoka kitabu cha Yohana Sura ya 8:32, akisema, “Kwa maana mtaifahamu ukweli, na ukweli utawaweka huru.

February 9, 2024