Tume ya JSC

Tume ya Huduma za Mahakama nchini (JSC) imeanzisha mchakato wa kumwondoa Jaji Mohammed Kullow wa Mahakama ya Mazingira na Arthi, kwa madai ya kuchelewesha na kushindwa kutoa maamuzi katika kesi 116.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatano 6.03.2024, JSC imethibitisha kwamba Jaji huyo alivunja mwongozo wa kimaadili na pia kukiuka katiba katika utendakazi wake, na hivyo kumtaka Kiongozi wa Taifa, Rais William Ruto, kuunda jopo la kutathmini utendakazi wake kwa mujibu wa sheria.

SOMA PIA: JSC Yachapisha Majina ya 7 Wanaowania Wadhifa wa Msajili Mkuu wa Mahakama.

Kulingana na tume hiyo, tuhuma tatu kati ya tano dhidi ya Jaji huyo zimeonekana kuwa za kweli, hivyo kufanya mapendekezo ya kuondolewa kwake ofisini.

 

March 6, 2024