Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) imetangaza majina ya wagombea saba wanaowania wadhifa wa Msajili Mkuu wa Mahakama. Nafasi hiyo ilikuwa wazi baada ya Bi. Ann Amadi kuondoka mwezi jana baada yake kumaliza muhula wake wa miaka 10.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa JSC, Jaji Mkuu Martha Koome, saba hao watahojiwa tarehe 18 Machi mwaka huu, kabla ya JSC kumchagua atakayeijaza nafasi hiyo muhimu. Jumla ya watu 43 walituma maombi ya kujaza nafasi hiyo.
SOMA PIA: JSC) imetangaza majina ya wagombea saba wanaowania wadhifa wa Msajili Mkuu wa Mahakama. Nafasi hiyo ilikuwa wazi baada ya Bi. Ann Amadi kuondoka mwezi jana
Wagombea hao ni:
Rose Macharia Wachuka, Jack Ouma Mwimali, Fridah Boyani Mokaya, Anne Wambeti Ireri, Paul Ndemo Maina (ambaye kwa sasa anahudumu kama Kaimu Msajili Mkuu) Caroline Kendagor Jepyegen na Kennedy Kandet Lenkamai.
JSC has shortlisted candidates for the position of Chief Registrar of the Judiciary. The interviews will be conducted on 18th March 2024. pic.twitter.com/TSHLEEsF4V
— Judicial Service Commission Kenya (@jsckenya) February 16, 2024