BY ISAYA BURUGU 22ND JUNE,2023-Oparesheni ya kupambana na pombe haramu imengoa maeneo mbali mbali Narok kusini baada ya serikali ya kitaifa kuungana na serikali ya kaunti ya Narok kupambana na mihadarati.Ni hatua iliyoshabikiwa na wenyeji wengi wa eneo hilo ikizingatiwa kuwa pombe hiyo haramu imechangia kudorora kwa hali ya kiusalama,Watoto kutokwenda shuleni na maadili ya wanafunzi kudhoofika.Antony Mintila ana mengi.
Wenyeji wa eneo la Sogoo Narok kusini wameunga mkono hatua ya serikali kufanya oparesheni katika eneo la Narok kusini. Wakiongozwa Rev Matthew Chelule wameunga mkono hatua hiyo wakisema eneo hilo limegonga vichwa vya habari kwa unywaji na uuzaji wa pombe haramu.
Wakati uo huo wakazi hao wamelaani hatua ya baadhi ya wazee kina mama na vijana kujiingiza kwa unywaji wa pombe haramu hatua imepelekea idadi kubwa ya wanajamii kudorora kwa madhili.
Naibu kamishana wa eneo hilo Felix Kisalu amehaidi kushirikiana na wakazi wa eneo hilo wazee wa vijiji sawa machifu kukabiliana vikali na wagema Narok kusini. Kisalu amesema serikali itawakabili vikali wanywaji wa pombe haramu.