BY ISAYA BURUGU 20TH JAN 2023-Jumla ya watainiwa 173,345 waliokalia mtihani wa kitaiafa kwa kidato cha nne mwaka jana KCSE waliapata alama ya C chanya na Zaidi.
Haya ni kwa mjibu wa matokeo ya mtihani huo yaliyotanagzwa leo na Waziri wa elimu Ezekiel Machogu.Jumla ya watainiwa 1,146 walipata alama ya A. Waziri ametoa ripoti hiyo katika makao makuu ya baraza la mitihani nchini KNEC jijini Nairobi .
Tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali,ambapo mwanafuzni bora alitajwa, Waziri Machogu ametangaza tu jinsi gredi zilizovyosambazwa katika mtihani huo uliyofanywa na watainiwa 881,416 ambapo 443,644 walikuwa wanaume na 437,772 wakike
.Vilevile Waziri amefichua kuwa kama ilivyokuwa katika mtihani wa darasa la nane KCPE ,mwaka huu wizara imeafikia usawa wa kijinsia kwenye matokeo hayo kwani watainiwa wakike wlaifanya vyema swan a wenzao wakiume.
Wakati huo wataniwa wa KCSE mwaka jana walifanya vyema kwenye masomo 17 ikilingishwa na masomo 11 yaliyosajili matokeo yaliyoimarika mwaka 2021.
Idadi ya watainiwa waliopata alama ya E ilipungua mwaka jana na kufikia alfu 30822 mabayo inashiria asilimia 3.49 ikilinganishwa na wataniwa alfu 46251 ambayo ilikuwa ni asilimia 5.56 mwaka 2021.
waziri akisema kuwa matoke o yam waka jana ayanashiria kuwa kulikuwa na matokeo bora kiujumla hali ambayo itawapelekea wengi kujiunga na vyuo vya anuai nchini Watanaiwa wanaweza kupata matokeo yao kwa kutuma ujumbe mfupi kuanza na neno KCSE na kisha nambari yao ya usajili yaani index number kwa 20076.