Rais William Ruto amemteua Mbunge wa Mbeere Geoffrey Kiringa Ruku kuwa waziri wa Utumishi wa Umma na kuchukua nafasi ya Justin Muturi.
Tangazo hilo limetolewa katika taarifa na Mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei. Kwa miezi kadhaa sasa, Muturi amekuwaJustin Muturi afutwa kazi kama waziri wa utumishi wa umma. akimkosoa Rais William Ruto kutokana na visa vya utekaji nyara na mauaji ya waandamanaji wa Gen Z ambapo mwanawe pia alikuwa mwathiriwa.
Muturi alisema kwamba aliomba kutoshiriki vikao vya Baraza la Mawaziri hadi masuala ya utekaji nyara na mauaji ya kiholela yatakapopatiwa kipaumbele.
Wakati huo huo waziri wa mazingira Aden Duale amehamishwa hadi katika wizara afya huku Deborah Barasa ambaye ni waziri wa afya akihamishwa katika ile ya mazingira.
Vilevile rais amefanya uteuzi mpya katika baraza hilo ambapo Geoffrey Ruku ameteuliwa kama waziri mpya wa utumishi wa umma na Hanna Wendot ndiye waziri mteule wa Jinsia na tamaduni.
𝗣𝗥𝗘𝗦𝗜𝗗𝗘𝗡𝗧𝗜𝗔𝗟 𝗡𝗢𝗠𝗜𝗡𝗔𝗧𝗜𝗢𝗡𝗦 𝗧𝗢 𝗖𝗔𝗕𝗜𝗡𝗘𝗧 & 𝗣𝗢𝗥𝗧𝗙𝗢𝗟𝗜𝗢 𝗥𝗘-𝗔𝗦𝗦𝗜𝗚𝗡𝗠𝗘𝗡𝗧𝗦 pic.twitter.com/ao72Z2dq7g
— State House Kenya (@StateHouseKenya) March 26, 2025