Aliyekuwa Waziri wa Utumishi wa Umma Justin Muturi amekanusha madai kwamba kufukuzwa kwake kulitokana na utendakazi duni au kutohudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri.
Badala yake, anadai kuwa kuondolewa kwake kulihusishwa na misimamo yake kuhusu mauaji na utekaji nyara wa kiholela, masuala ambayo anadai yamevuruga utawala wa Rais William Ruto.
Akizungumza katika kikao na wanahabari siku ya Jumatano, Muturi alisema kuwa kutimuliwa kwake ni matokeo ya moja kwa moja ya wito wake wa kutaka serikali kushughulikia visa vya watu kutoweka na kuuwawa.
Aidha alidai kuwa washirika wa karibu wa Rais wamekuwa wakishinikiza ajiuzulu kutokana na msimamo wake thabiti kuhusu suala hilo.
Muturi alifichua kwamba alialikwa kwenye mkutano wa mwisho wa Baraza la Mawaziri uliofanyika Machi 11 katika Ikulu ya rais lakini alichagua kutohudhuria.
I DID NOT ABSCOND, RUTO FIRED ME OVER MY STAND ON EXTRA JUDICIAL KILLINGS
The President in a televised interview on the night of 31st March 2025 at Sagana State lodge stated that I was relieved of my duties for failing to attend cabinet meetings. I would wish to respond as… pic.twitter.com/ftdcgIx7Zy
— Hon. Justin Muturi, EGH (@HonJBMuturi) April 2, 2025