Kamati ya Bunge inayoshughulikia masuala ya Mawasiliano na Teknolojia imeanzisha uchunguzi kuhusu usalama wa taarifa za wananchi waliosajiliwa na kampuni ya sarafu za kidijitali ya World Coin. Chini ya uongozi wa Mbunge wa Dagoretti Kusini, John Kiarie, kamati hiyo imemhoji Kamishna wa Ulinzi wa Taarifa, Immaculate Kassait mapema leo.
Lengo la mazungumzo hayo lilikuwa kufahamu kama Kamishna Kassait alikuwa na ufahamu wa shughuli za Worldcoin nchini Kenya, mfumo wa kisheria ambao kampuni hiyo inaendesha shughuli zake, na pia kubainisha nani aliyeidhinisha ukusanyaji wa data kutoka kwa raia wa Kenya.
The Departmental Committee on Communication, Information and Innovation chaired by Dagoretti South MP, Hon John Kiarie (@KiarieJohn) is currently meeting the Data Protection Commissioner Immaculate Kassait.
The committee is seeking answers on the collection of private citizens’… pic.twitter.com/gZfoKcWS5q
— National Assembly KE (@NAssemblyKE) August 15, 2023
Hapo awali, ofisi ya Kamishna wa Ulinzi wa Taarifa za Kibinafsi nchini (ODPC) ilieleza kwamba imewasilisha ombi kwa Mahakama la kuiagiza Kampuni ya sarafu za kidijitali ya Worldcoin kuzuia upatikanaji au matumizi ya Taarifa za Binafsi ilizokusanya kutoka kwa raia wa Kenya.
ODPC imesema kuwa Worldcoin imekiuka Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa kukusanya taarifa hizo kwa njia isiyofuata sheria na kuna wasiwasi kwamba wanaweza kuzihariri au kuzifuta ili kuficha ushahidi.