BY ISAYA BURUGU 30TH AUG 2023-Miungano ya Kenya Kwanza na Azimio la Umoja imekubali kuruhusu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kuendelea na majukumu yake.Wakizungumza katika ukumbi wa Bomas hivi leo Timu hiyo inayoongozwa na kinara wa Wiper Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka na Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wah ilisema kuwa jukumu la jopo hilo halitaingiliwa.Hata hivyo, Ichung’wah alisema kuwa kufanya hivyo hakuzuii kamati hiyo kujadili masuala yanayohusu IEBC, na hivyo basi, wameandikia jopo ilani ya mahakama, kuwaarifu kuhusu kutendeka kwa kamati hiyo.Mbunge huyo wa Kikuyu aliongeza kuwa jopo la IEBC litakuwa miongoni mwa washikadau walioalikwa wakati kamati hiyo itakapoanza mazungumzo na washikadau
.Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka alisema jopo la IEBC ambalo jukumu lake ni kuajiri mwenyekiti na
Makamishna sita wa IEBC wanaweza kusikia kutoka kwa kamati ya mazungumzo.Alisema kamati ya mazungumzo imeweza kupiga hatua zitakazoongoza mchakato wa mazungumzo katika siku 59 zijazo