Kamishna wa kaunti hii ya Narok Isaac Masinde amezuru mpaka wa Nkararo na Enoreteet kule Transmara ambapo mzozo umekuwa ukiendelea kwa siku nne mfululizo.

Mzozo huo umesababisha uharibifu wa mali huku nyumba kadhaa zikiteketezwa. Jamii za Isiria na irwasingishu zimekuwa zikizozania mpaka huo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Bw. Masinde ameeleza kuwa usalama umeimarishwa katika eneo hilo na kufikia sasa wamefanikiwa kuwatia mbaroni watu 22 wanaodaiwa kuanzisha moto huo.

June 7, 2023