BY ISAYA BURUGU 22ND NOV 2022-Serikali ya kaunti ya Kisumu imezindua mkakati wa utoaji huduma msingi za kiafya unaotilia maanani kuzuia magonjwa huku washirika wakiitisha kutengewa fedha Zaidi za mpango huo.Mpango huo wa miaka miwili unatokana na na mpango wa kitaiafa wa uboreshwjai wa afysy msningi wa kati yam waka 2019-2024.
Dakita Kennedy Otieno, ambaye ni naibu kurugenzi mkuu wa huduma za kiafya kwenye kaunti hiyo amesema kuwa asilimia 80 ya magonjwa yanaweza kukabiliwa kikamilifu kwenye kiwnago cha nyumba .Otieno amesema hospitali zitaendelea kutoa huduma zake za kuponya lakini magonjwa mengi yanaweza shughulikiwa nyumbani .
Mmmoja wawashiriki wakuu katika kubuni mkakati huo Patricia Orao, ambaye ni mkurugenzi mkuu wa shirika la stawisha Dada amesemaa afya bora inapaswa kuwa jukumu na shabaha ya kila mkenya.
Akizungumza na wandishi Habari wakati wa uzinduzi wa mpango huo jijini Kisumu Oraro amesema mkakati huo unalenga kuhakikisha kuwa kila mtu katika kiwango cha familia anachukua udhibiti wa Maisha yao ili kujiepusha na matumizi ya kiwango cha juu cha kifedha kusaka matibbau.