BY ISAYA BURUGU 28TH AUG 2023-Serikali kupitia wizara ya vyama vya ushirika na biashara nchini imetenga shilingi bilioni 3.8 kwa lengo la kuimarisha sawa na kupanua viwanda vya maziwa vya KCC katika maeneo tofauti humu nchini.Kaunti ya Narok imetengewa shilingi milioni 700 za kujenga kiwanda kipya cha maziwa kwenye ardhi ya ekari 30 iliyotengwa na serikali ya kaunti ya Narok kufanikisha ujenzi huo.

Haya yamesemwa na  waziri wa vyama vya ushirika na biashara nchini Simon Chelugui akiongea katika ziara yake kwenye kaunti ya Narok ambapo amesema kwamba baada ya serikali kuimarisha na kupanua viwanda vya maziwa humu nchini taifa la Kenya litakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 4.5 ya maziwa kila siku kutoka kwa lita 1.5 ya sasa.

Hivyo basi amewataka wananchi kuingilia ufugaji wa ngombe wa kisasa ili waweze kunufaika kupitia biashara hiyo ya maziwa.Waziri huyo kadhalika amedokeza kwamba serikali inaangazia pia swala la bei ya maziwa ambapo anasema kila lita ya maziwa itakuwa inauzwa kwanzia shilingi 50

.

Hatua hiyo imeshabikiwa na gavana wa Narok Patrick Ntutu.

.

August 28, 2023