BY ISAYA BURUGU,30TH OCT,2023-Kaunti za Uasin Gishu na Elgeyo Marakweti zimeorodheshwa kuwa kaunti bora Zaidi katika utenda kazi. Utafiti uliotolewa leo na Infotrak uliwapa Pokot Magharibi alama ya wastani ya asilimia 87 ikifuatiwa na Elgeyo Marakwet kwa asilimia 83 na Tharaka Nithi (asilimia 80).
Kaunti zingine zilizoorodheshwa kuwa zilizofanya vyema katika maendeleo ni pamoja na Embu iliyopata alama 80, Homa Bay 79 (asilimia), Bomet (asilimia 78), Kericho (asilimia 77), Laikipia na Kirinyaga (asilimia 76).
Kajiado (asilimia 75) na Makueni (asilimia 75).Kaunti za Trans Nzoia, Vihiga, Meru, Machakos na Kisii zilipata asilimia 74.
Utafiti huo ambao ulifanywa kati ya Julai na Agosti 2023, ukihusisha kaunti zote 47, maeneo bunge 290 na wadi 1450 zilizo na sampuli ya jumla ya 36,200 pia uliainisha utendakazi wa kaunti kulingana na kazi mbalimbali zinazoendeshwa na serikali za kaunti. Angela Ambitho ni mkuregenzi mkuu wa Shirika hilo.