Baraza la maaskofu wa Kanisa Katoliki limetaka mazungumzo yafanyike kati ya Rais William Ruto na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, ili kuepusha mzozo unaojitokeza.
Wakihutubia wanahabari Maaskofu hao wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza hilo askofu mkuu Martin Kivuva, wamemsihi Rais Ruto atimize ahadi yake ya kuketi na kufanya mazungumzo na mpinzani wake wa kisiasa ili kutatua masuala.
Wakati uo huo, wamemrai Bw. Odinga kukubali mazungumzo kama njia ya kusuluhisha mzozo uliopo.
Pia wamewashauri washirika wa Raila, akiwemo Martha Karua na Kalonzo Musyoka, kusitisha maandamano yanayopangwa kila wiki wakidai kuwa si kupigana vifua wala kuelekeza lawama kutasuluhisha machafuko ambayo Kenya inashuhudia.