BY ISAYA BURUGU,26TH JAN 2023-Mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya CA imetoa takwimu mpya za utafiti wa matumizi ya mitandao ya kijamii katika ukanda wa Afrika Mashariki.Katika utafiti huo, Kenya na Tanzania kuenea kwa mawasiliano ya mtandao wa simu za mkononi unafuata nyuma ya Uganda, ambayo ina kiwango cha juu zaidi cha kupenyeza kwa mtandao wa simu za mkononi.
Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) zinaonyesha Uganda ilikuwa na upenyaji wa mtandao wa simu wa asilimia 46.88 kufikia Juni 2021 na kushinda asilimia 46.76 ya Kenya.
Sudan Kusini ilikuwa ya mwisho kati ya nchi hizo sita, Burundi ilikuwa ya pili kwa kiwango cha chini cha upenyaji wa mtandao wa simu wa asilimia 10.96 huku Rwanda na Tanzania zikiwa na asilimia 42.84 na asilimia 14.31 mtawalia.
Haya yanajiri licha ya Kenya kuzishinda nchi nyingine za EAC katika kupenya kwa simu za rununu.Simu za rununu zilifikia asilimia 114 katika kipindi hicho ikilinganishwa na asilimia 61 tu nchini Uganda, asilimia 86 nchini Tanzania na asilimia 82 nchini Rwanda.