Siku ya leo, Kenya inaungana na mataifa mengine kote ulimwenguni katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utamaduni na Tofauti za Kijamii. Maadhimisho haya, ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 21 Mei tangu mwaka wa 2005, yananuia kusherehekea utofauti wa kijamii na kuimarisha mahusiano kati ya jamii mbalimbali ili kuhakikisha maendeleo endelevu.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), utamaduni ni moja ya vichocheo vikubwa zaidi vya maendeleo. Ripoti hiyo inaeleza kwamba sekta hii inachangia kwa takriban nafasi milioni 48 za ajira ulimwenguni, ikiwa ni mojawapo ya sekta zinazowaajiri vijana walio chini ya miaka 30 kwa idadi kubwa zaidi.
SOMA PIA: Gavana Ntutu Awataka Kina Mama Kuongoza Vita Dhidi ya Mimba na Ndoa za Mapema
Siku hii ni fursa muhimu kwa Kenya na mataifa mengine kufikiria na kuhamasisha njia za kushirikiana na kutumia utofauti wa kijamii kama nguvu ya maendeleo.