BY ISAYA BURUGU,11TH APRIL,2023-Murengo wa Kenya Kwanza umezindua jopo lake la watu saba litakaloshiriki mazungumzo ya Pamoja ya bunge na upande wa upinzani.Kwenye mkao na wandishi Habari,kinara wa wengi katika bunge la kitaiafa Kimani Ichung’wa amesema kuwa wabunge hao walichaguliwa kufuatia mazungumzo yaliyoandaliwa mapema na kundi la wabunge tekelezi wa Kenya Kwanza.
Waliochaguliwa ni seneta wa kakamega Boni Khalwale, mwenzake wa Bomet Hillary Sigei, seneta mteule Essy Okenyuri, mwakilishi wakike kaunti ya Taita Taveta Lydia Haika, mbunge wa Tharaka George Murugara, mbunge wa Kibwezi West Mwengi Mutuse, na mbunge wa Edlas MP Adan Keynan Ichung’wa amesema kuwa wamekubaliana na President William Ruto kuhusu umuhimu wa kuongoza taiafa hili kwa kufuata mkondo wa sheria na kushirikiana na upinznaini kwa manufaa ya taifa hili
.Ichungwa hata hivyo amesisitiza kuwa jopo hilo halina mpango wa kushughulikia sharti la Azimio kutaka IEBC kufungua Sava.
.Wiki iliyopita murengo wa Azimio ulizindua wawakilishi wake kwenye mazungumzo hayo ambao ni Narok Senator Ledama Ole Kina, Nairobi Senator Edwin Sifuna, Makueni Senator Enock Wambua, MPs Millie Odhiambo (Suba North), Amina Mnyazi (Malindi), David Pkosing (Pokot South), and Otiende Amollo (Rarieda).