Kenya Iran

Rais William Ruto amemkaribisha Rais Ebrahim Raisi wa Iran katika ikulu ya Nairobi, ambapo viongozi hao wameahidi kuimarisha ushirikiano kati ya Kenya na Iran katika sekta mbalimbali za kiuchumi na masuala mengine.

Katika mkutano wao, Rais Ruto na Rais Raisi wamezungumzia umuhimu wa kuendeleza mahusiano ya kidiplomasia kati ya Kenya na Iran. Viongozi hao wawili wamejadili mikakati ya kukuza biashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili na kusaini makubaliano kadhaa yanayolenga kuimarisha shughuli za kibiashara, ukulima, elimu na maeneo mengine.

Katika hotuba yake rais Ruto amesisitiza umuhimu wa ushirikiano huu katika kukuza uhusiano wa Kenya na Iran na kuimarisha maslahi ya pande zote. Aidha, ameelezea matumaini kuwa ushirikiano wa karibu kati ya Kenya na Iran utasaida kufungua milango ya kibiashara katika masoko ya Afrika na Asia.

Rais Raisi wa Iran kwa upande wake amepongeza juhudi za Kenya katika maendeleo ya kiuchumi na kusisitiza nia ya Iran kuimarisha uhusiano huo kupitia ushirikiano wa kibiashara, uwekezaji na masuala ya kiufundi. Ameelezea matarajio yake ya kuona uhusiano huu ukiendelea kukua na kuleta manufaa kwa raia wa nchi hizi mbili.

https://twitter.com/StateHouseKenya/status/1679035659141410817?s=20

 

July 12, 2023