BY ISAYA BURUGU,14TH MARCH,2023-Rais wa Italia Sergio Mattarella HIVI LEO amekutana na rais Wiliam Ruto katika ikulu ya Nairobi.Rais Matarrela yuko humu nchini kwa ziara ya siku mbili.Katika mkutano kati ya viongozi hao wawili,mikataba miwili imetiwa Saini itakayowezesha Kenya na Italia kushirikiana katika Nyanja mbali mbali.Wa kwanza unahusu kusaidia Kenya katika kufanikisha mpango wa utoaji huduma bora za kiafya kwa wote maarufu kama UHC huku pia serikali ya italia ikikubali kusaidia Kenya kuanza ujenzi upya wa mabwawa ya Kimwarer,na Aror katika kaunti ya Elgeyo marakweti,miradi ambayo ilisitishwa kufuatia agizo la mahakama
.Viongozi hao wawili pia wameafikia kuondoa vikwazo vya usafiiri na kibaishara kati ya nchi hizi mbili ili kupiga jeki utangamano na baishara..
Kwa upande wake rais Mattarella amesema kuwa Italia inachukulia Kenya kuwa taiafa lililostawi Zaidi kidemokrasia,na lilo na mazingira bora ya uwekezaji na kuahidi kuwa nchi yake itazidi kushirikiana na Kenya kwenye Nyanja tofuati kwa minajili ya manufaa ya raia wan chi hizi mbili.