Rais William Ruto hii leo amekuwa mwenyeji wa waziri mkuu wa Singapore Lee Loong ambapo wamekubaliana kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili.

Kwenye kikao cha pamoja na waandishi wa habari, wawili hao wamesema kuwa wataweka mikakati itakayohakikisha kuwa wawekezaji wa Singapore wanawekeza humu nchini ili kuimarisha mauzo ya nje ya mataifa yote mawili.

Waziri mkuu Loong aliongeza Asia Kusini, inayoundwa na nchi 10 na yenye wakazi takriban Milioni 670, inaipa Kenya soko “la kipekee na kubwa” la kuuza bidhaa zake.

 

May 18, 2023