Mataifa ya Kenya na Ujerumani yamekubaliana kuweka kipaumbele mikakati ya kuondoa vizuizi visivyo vya ushuru kati ya mataifa haya mawili ili kukuza biashara.

Hatua hiyo inadhamiria kupunguza gharama za biashara na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na huduma kati ya mataifa haya. Rais William Ruto ambaye yuko ziarani katika taifa la Ujerumani alisema kuondolewa kwa vikwazo hivi pia kutawawezesha wawekezaji kutoka ujerumani kuingia katika soko la Kenya.

Rais Ruto alikua akizungumza alipokutana na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier huko Schloss Bellevue, Berlin. Viongozi hao wawili waliahidi ushirikiano wa kina wa kiuchumi kwa ajili ya ustawi Kenya Na Ujerumani.

March 27, 2023