Kenya imeanza shughuli ya kuwaondoa wananchi wake kutoka nchi ya Sudan kunakoendelea vita vya kisiasa.

Kenya imekuwa mojawapo ya nchi ambazo zimewaondoa wananchi wake kutoka nchi hiyo kutokana na makabiliano makali baina ya jeshi la Sudan na kikundi cha Paramilitary Rapid Support Forces.

Mapigano hayo yameingia wiki ya pili tangu kuanza.Baadhi ya mataifa ambayo yamewaondoa raia wake ni pamoja na Marekani, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani na Canada ambayo tayari yalianza shughuli hiyo.

Waziri wa masuala ya nje Dkt Alfred Mutua alitangaza kuwa  mataifa jirani  yakiwemo Sudan, Ethiopia, Misri na Saudi Arabia yameipa Kenya ruhusa ya kutumia anga zao kuwasafirisha Wakenya walio nchini Sudan.

Mutua alisema kuwa wizara ya mambo ya nje tayari ina programu tatu zinazoendelea za kuwatoa wananchi wa Kenya kutoka Sudan.

Tayari, Wakenya  29 ambao ni wanafunzi wamevushwa kwenda Uhabeshi ambapo wataenda sehemu ya Gondor , Addis Ababa kisha Nairobi.

Mutua aliongezea pia kuwa Wakenya wapatao 200-300 wataondolewa Sudan kupitia mpango huu.Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kuwa watu zaidi ya 400 wameripotiwa kufa kutokana na vita hivyo  huku maelfu waijeruhiwa.

April 25, 2023