Kenya inajitahidi kushirikiana na Umoja wa Falme za Kiarabu kupiga jeki mpango wa lishe shuleni ili kuongeza idadi ya watoto wanaonufaika na mpango huo.

Haya ni kwa mujibu wa Naibu Rais Rigathi Gachagua.Akizungumza alipomkaribisha Waziri wa Mazingira na Mabadiliko ya Hali ya Hewa wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mariam Almheiri, Gachagua alisema Kenya inalenga kufanya kazi na UAE kupanua mpango huo.

Naibu Rais alisisitiza kwamba Kenya inafuata hatua za mataifa mengine kama vile UAE ambayo yamefaulu katika mpango huo wa lishe shuleni.

Hali kadhalika alisema kuwa serikali inapania kuongeza idadi ya watoto wa shule chini ya mpango huo kutoka Milioni 1.8 hadi milioni 10 ifikapo mwaka wa 2030.

September 4, 2023