Wakenya waliraiwa kushiriki katika shuguli za uhifadhi wa mazingira kama vile upanzi wa miche na shuguli zingine za usafi wanaposherehekea siku kuu ya mazingira.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusherehekea siku hii katika bustani ya Arboretum, Waziri wa mazingira Aden Duale, alifichua kuwa Wakenya wamepanda miti milioni 481 kuanzia Januari 2024, akisisitiza juhudi za pamoja katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga.

Duale alipongeza umma kwa kushiriki katika mpango wa serikali wa kupanda miti bilioni 15 kufikia 2032.

Kando na hayo, Duale alirejelea mpango wa kusafisha mto Nairobi ambapo alisema kuwa watashirikisha vijana 20,000 kutoka kaunti ya Nairobi huku akitoa onyo kwa kampuni zinazochangia uchafuzi wa mazingira.

October 10, 2024