BY ISAYA BURUGU,16TH JUNE,2023-Kenya inaungana na ulimwengu hivi leo kuadhimisha siku ya mtoto wakiafrika.Katika kauntihii ya Narok maadhimisho hayo yanandaliwa katika uwanja wa Wiliam Ole Ntimama Mjini Narok huku Zaidi ya Watoto mia tatu kutoka shule mbali mbali wakihudhuria.
Kunao pia maafisa kutoka vitengo mbali mbali vya kuwatunza Watoto waliokusanyika kwa maadhimisho hayo. Pilot Khaemba ambaye ni afisa wawatoto kaunti ya Narok amezungumza na radio Osotua katika kipindi cha DIRA YA KAZI kuhusu umuhimu wa siku ya leo.
.Afisa huyo akiguzia umuhimu wa kauli mbiyu ya maadhimisho ya mwaka huu.
Wakati huo huo `maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kaunti ya Nakuru yameandaliwa katika kaunti ndogo ya NJoro. Agnes Magina ambaye ni afisa wa watoto kaunti ndogo ya njoro anasema siku hii ni muhimu haswa kwa kuzingatia changamoto mbali mbali zinazomkumba mtoto mwafrika.
Baadhi ya changamoto hizo ni dhulma za kimapenzi,dhulma kupitia njia za mitandao n ahata kunyimwa haki zao msingi
.