BY ISAYA BURUGU 03,MAY 2023-Wadau mbali mbali katika sekta ya uandishi Habari  wanakutana hivi leo katika hoteli ya Safaripark jijini Nairobi kuadhimisha siku ya uhuru wa wanahabari ulimwenguni. Siku hii huadhimishwa tarehe tatu mwezi Mei Kila mwaka.

Madhimisho ya mwaka huu yanayongozwa na baraza la vyombo vya Habari nchini yanafanyika wakati visa vya dhulma dhidi ya wandaishi Habari humu nchini vinazidi kushudiwa. Katika siku za hivi karibuni matukio ya kuvamiwa na kujeruhiwa kwa wandishi Habari wakiwa kazini yameripotiwa humu nchini.

Baadhi ya visa hivyo ni uvamizi wa wanahabari wanaoangazia mandamano ya mungano wa Azimio La umoja  dhidi ya serikali huku visa kadhaa vikiripotiwa tangu kuanza kwa mandamano hayo.Vilevile kunyimwa fursa ya kuangazia yanayofanyika katika shamba la Shakahola kule Kilifi ambapo Zaidi ya miili 100 ya wafuasi wa dhehebu la Good News International imepatikana.

Mwenyekiti wa chama cha wahariri nchini Zubeida Koome akizungumza kwenye hafla hiyo amesisitiza haja ya serikali kuhakikisha wandishi Habari wanafanya kazi kwa mazingira yenye amani bila vitisho .

Kuendelea kupungua kwa mapato kunaokumba mashirika mengi ya Habari kumewadhiri wandishi wa Habari huku mishara ikichelewa hali ambayo Koome anasema  ni sharti juhudi sisizokuwa za kawaida kufanywa na wahusika wote kusaka suluhu

.Kauli mbiyu ya maadhimisho yam waka huu ni haki za wanahabari kwa siku zijazo.

 

May 3, 2023