BY ISAYA BURUGU,12TH MAY 2023-Huku Kenya ikiungana na ulimwengu hivi leo kuadhimisha siku ya wauguzi duniani hivi leo,wauguzi katika kaunti ya Nyamira wamelalamikia mazingira duni ya utenda kazi.

Wakizungumza katika hospitali ndogo ya Masaba kaskazini mjini Keroka,wauguzi hao wamelalamikia kucheleweshwa kwa mishahara na marupurupu yao,

kutopandishwa vyeo kwa muda mrefu na kutoongezwa kwa mishahara kwa muda mrefu, na kutoangezwa kwa mishara ya wauguzi ambao tayari wamepandisha vyeo.

Viongozi wa wizara ya afya katika kaunti hiyo wametoa hakikisho kuwa wataluhisha swala hilo ili kuhakikisha kuwa mishara inalipwa kwa wakati unaofaa.

May 12, 2023