Kinara wa upinzani Raila Odinga amedai kuwa makosa yaliyorekodiwa katika matokeo ya mtihani wa KCPE ya mwaka 2023 yaliyotolewa hivi majuzi yana mzozo mkubwa wa ununuzi katika Wizara ya Elimu.

Akihutubia wanahabari jijini Nairobi, Odinga alisema mnamo 2016, kampuni moja ya Uingereza ilipewa zabuni ya kuchapisha mitihani hiyo baada ya wasiwasi kuhusu uadilifu wa mitihani ya kitaifa huku akidai kuwa zabuni hiyo ilikatishwa ghafla na serikali ya sasa kwa sababu kampuni hiyo ilikataa kutoa pesa.

Aidha aliomba uchunguzi wa kina ufanywe kuhusu utoaji wa zabuni hiyo kwa kampuni inayodaiwa kuwa katika eneo la Mombasa Road na kutaka Wakenya waelezwe jinsi tuzo hiyo ilivyoafikiwa.

December 6, 2023